Miili ya wahajiri 11 yapatikana ufuoni mjini Tripoli, Libya
Habari zaidi zinasema kuwa, wahajiri hao walikuwa wanakusudia kuelekea nchini Italia kwa kutumia boti ndogo za plastiki, kupitia Bahari ya Mediterranea.
Hivi karibuni, Shirika la Kimataifa la Uhajiri (IOM) lilisema wakimbizi na wahajiri wapatao 5,000 wamepoteza maisha mwaka huu wa 2016 wakijaribu kuingia barani Ulaya kupitia Bahari ya Mediterranea.
Joel Millman, msemaji wa shirika hilo amesema idadi hiyo imeongezeka baada ya watu 100 kufa maji Alkhamisi iliyopita, baada ya boti mbili walizokuwa wakisafiria kuzama katika Lango la Sicily, kati ya Italia na Libya.
Naye William Spindler, msemaji wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR amesema kiwango hicho cha vifo baharini mwaka huu kimevunja rekodi na kwamba hakuna mwaka ambao umewahi kushuhudia vifo vya wahajiri baharini kiasi hiki.
0 comments: