TINGATINGA LA WIZARA YA ARDHI LABOMOA NYUMBA BONDE LA MKWAJUNI WILAYANI KINONDONI, DAR ES SALAAM

 NYUMBA na vibanda kadhaa vilivyojengwa kwenye eneo "hatarishi" la bonde la mto Msimbazi maeneo ya Mkwajuni jijini Dar es Salaam, zimebomolewa leo Desemba 17, 2015, baaa ya maafisa wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makzi, wakiwa na tingatinga kufanya kazi hiyo iliyoacha vilio kutoka kw waliokua wamiliki wa nyumba na vibanda hivyo. Hatua hiyo inachukuliwa ikiwa ni jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kuchukua tahadhari ya kujiepusha na madhara yatokanayo na mafuriko ambapo kwa hakika eneo lote la bonde la Msimbazi takriban kila mwaka hukumbwa na madhara makubwa yanayoambatana na vifo vya watu kutokana na mafuriklo. Pichani Tingatinga hilo likiwa kazini


0 comments: