WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI AZINDUA “MAGEREZA DUTY FREE SHOP” GEREZA KEKO PAMOJA NA KIWANDA CHA KUTENGENEZA MABAKULI YA WAFUNGWA GEREZA UKONGA, JIJINI DAR ES SALAAM

image_4Mabakuli na vikombe ambavyo vitakuwa vikitengenezwa katika Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga. Vifaa hivyo mabakuli na vikombe vitatumiwa na Wafungwa waliopo Magerezani kulia chakula. Katika picha anayeonekana ni Mpiga picha wa Jeshi la Magereza, Mkaguzi wa Magereza, Deodatus Kazinja akiwajibika ipasavyo wakati wa uzinduzi rasmi wa Kiwanda hicho, Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam. image_1Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza waliohudhuria hafla fupi ya uzinduzi wa Magereza Duty Free Shop ya Gereza Keko, Jijini Dar es Salaam wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(hayupo pichani).imageKamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kwa Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(wa tatu kulia) kabla ya kumkaribisha rasmi kwa uzinduzi wa Magereza Duty Free Shop ya Gereza Keko (wa kwanza kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Tuhaferi. image_3Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kiwanda cha kutengeneza Bakuli na Vikombe vitakavyokuwa  vinatumika na Wafungwa Magerezani kulia chakula(wa kwanza kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja.
photoWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(kushoto) akiwaonesha Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dar es Salaam jiwe la msingi la Jengo la Magereza Duty Free Shop iliyopo Gereza Keko, Jijini Dar es Salaam(kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja. Uzinduzi huo wa Magereza Duty Free Shop umefanyika juzi katika eneo la Gereza Keko.

0 comments: